Huwezi kusikiliza tena

Ndoto ya Afrika yabisha Nigeria

Kama sehemu ya makala ya BBC Ndoto ya Afrika, mtengezaji muziki, Cobhams Asuquo, anatusimulia namna ambavyo, amekuwa mmoja wa wasanii mashuhuri nchini Nigeria.

Cobhams amekuwa kipofu tangu kuzaliwa na ameweza licha ya ulemavu wake kuwa mmoja wa wasanii wanaosakwa sana na wanamuziki barani Afrika.

Ameshirikiana na wasanii mashuhuri Nigeria wakati akikuza vipaji vya wanamuziki wa kizazi kijacho.

Anajivunia kuchangia muziki wake na dunia nzima.