Huwezi kusikiliza tena

Je wakenya wamesameheana?

Watu wengi wameachwa wakiuguza majeraha baada ya ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007 nchini Kenya ambapo zaidi ya watu elfu moja waliuawa na wengine zaidi ya laki mbili kuachwa bila makao kufuatia uchaguzi uliokumbwa na utata.

Mji wa Kisumu, ulioko Magharibi mwa nchi, ulikuwa moja ya miji iliyoathirika vibaya zaidi kutokana na vita. Kisumu ni nyumbani kwa Waziri mkuu Raila Odinga.

Juhudi zimefanyika huko kuwahamasisha watu kusameheana miongoni mwao lakini bado kuna hofu imetanda. Mwandishi wa BBC Ann Mawathe alizuru Kisumu na kuandaa taarifa hii.