Mkondo wa mwisho wa kampeini Kenya

Hii leo ni siku ya mwisho ya kampeini za uchaguzi mkuu nchini Kenya kabla ya uchaguzi kufanyika Jumatatu.

Utakuwa uchaguzi wa kwanza tangu ghasia kukumba nchi hiyo mwaka 2007 kufuatia utata ulioibuka kuhusu mshindi wa uchaguzi huo.

Ghasia zilisababisha vifo vya zaidi ya watu elfu moja na maelfu wengine kuachwa bila makao.

Ushindani mkali uko kati ya Waziri mkuu Raila Odinga na Naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta ambaye ni mshukiwa mkuu wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007 katika mahakama ya ICC.