Marehemu Hugo Chavez azikwa

Mwili wa marehemu Rais wa Venezuela Hugo Chavez umepitishwa kwenye umati mkubwa wa wafuasi wake katika mitaa ya mji mkuu Caracas.

Watu wengi waliangua kilio huku wakichukua picha za kiongozi wao aliyefariki dunia .

Mama yake na watoto wake walikusanyika mbele ya jeneza kutoa heshma zao .