Huwezi kusikiliza tena

Msimao wa AU kuhusu uchaguzi wa Kenya

Waangalizi wa uchaguzi nchini Kenya wameitakla tume ya uchaguzi kuonyesha uwazi katika shughuli inayoendelea ya kuhesabu kura za urais katika ukumbi wa Bomas.

Wanasisitiza hili kama hatua ya kutaka kuondoa wasiwasi wowote kuwa shughuli hiyo imehujumiwa.

Waangalizi waliyasema hayo hapo jana baada ya muungano wa CORD unaoongozwa na Raila Odinga kusema kuwa watakwenda mahakamani kuitaka mahakama kusitisha shughuli ya kutangaza matokeo kwa kutumia mfumo wa zamani. Hii ni baada ya mitambo ya tume ya uchaguzi ya kupeperusha matokeo kugoma.

Mmoja wa waangalizi ni Joachim Chisano, mwenyekiti wa kikosi cha waangalizi kutoka Muungano wa Afrika.