Huwezi kusikiliza tena

Jee Afrika itatoa mwanamke wa kwanza?

Hivi karibuni Shirika la Biashara Duniani WTO itafanya uchaguzi wake wa kumchagua mkurugenzi mkuu wa shirika hilo.

Kuna watu tisa wanaogombea kiti hicho wawili kati yao ni waafrika, Mghana na Msomi kutoka Kenya Bi Amina Mohamed

Salim Kikeke alizungumza naye na kumuuliza kwanini anafikiri kuwa yeye anastahili kuongoza shirika hilo la WTO.