Huwezi kusikiliza tena

Mkono wa buriani kwa Bi Kidude

Visiwani Zanzibar, msanii mkongwe, Bi Kidude alizikwa mnamo Alhamisi baada ya kufariki dunia.

Bi Kidude alikuwa na vipaji vya aina mbali mbali vilivyompatia umaarufu kote duniani ikiwa ni pamoja na kuimba, kupiga ala na hata kufundisha unyago mabinti waliojiandaa kuolewa.

Mwandishi wetu Hassan Mhelela ametuandalia taarifa hii kutoka Unguja.