Huwezi kusikiliza tena

Waigiza pingu za maangamizi Kenya

Nchini Kenya, kilele cha mashindano ya kuigiza kwa shule za msingi, sekondari na vyuo, katika ngazi ya kitaifa kilifika Jumapili jioni, kwa onyesho la mchezo wa kuigiza uliozua utata. Mchezo huo uliandaliwa na shule ya ulipili ya wasichana ya Butere kutoka Magharibi ya Kenya.

Mchezo huo Shackles of Doom au Pingu za maangamizi, ulipigwa mafuruku na wizara ya Elimu kwa madai ya kuchochea chuki za kijamii lakini Mahakama ikabatilisha uwamuzi wa maafisa wa elimu. Kwa nini basi Shackles of Doom ilionekana kuzua utata.

John Nene alikuwa kwenye fainali hizo mjini Mombasa na kujionea mchezo wa Wasichana wa Butere na hii hapa taarifa yake.