Huwezi kusikiliza tena

Kutana na Toya de Lazy wa Afrika Kusini

Toya de Lazy amefunzwa kucheza mziki wa jazz hasa akicheza Piano, lakini sasa mwanamuziki huyu pamoja na kuwa mtunzi anatifua kivumbi nchini Afrika Kusini kwa kucheza muziki wake aina ya electro-pop.

Mbwembwe zake pamoja na sauti yake ya ninga, vimeufanya muziki wake kuenziwa mno.

Kuna siri ndani ya jina lake kuwa yeye ni mwanawe aliyekuwa Chifu wa Zulu na mwanzilishi wa chama cha Inkatha Mangosuthu Buthelezi Albamu yake ya kwanza Due Drop, ilitolewa Aprili mwaka 2012.