Huwezi kusikiliza tena

Nini huvutia Mmbu kwa mwili wa binadamu?

Idadi ya watu wanaofariki kutokana na Malaria imeshuka kwa robo katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, lakini watu milioni 200 huugua ugonjwa huo kila mwaka.

Kwa muda tumekuwa tukifahamu kuwa Mmbu wenye vimelea vya Malaria huvutiwa na harufu ya mwili wetu. Lakini sasa watafiti wamegundua jambo moja lenye kutia wasiwasi , kuwa Mmbu wenye vimelea vya Malaria huvutiwa zaidi na harufu ya mwili wa bindamu kuliko wasio na vimelea hivyo.