Huwezi kusikiliza tena

Wahusika wa dhulma Kenya wawajibishwe

Baada ya tume ya Ukweli, Haki na Maridhiano nchini Kenya kumkabidhi Rais Uhuru Kenyatta ripoti yake hapo jana, waathiriwa wa ukiukwaji wa haki za kibinadamu nchini humo wamekuwa wakielezea maoni yao, huku baadhi wakionyesha mashaka kuhusu utekelezwaji wake, licha ya hakikisho kutoka Rais.

Ripoti hiyo imewataja wanasiasa wanaoshukiwa kuhusika na ukiukwaji haki, na inapendekeza wafunguliwe mashtaka.

Pia imemtaka rais kuomba msamaha kwa Wakenya wote walioathirika tangu nchi hiyo ilipopata uhuru. Anne Soy ametembelea kambi moja ya wakimbizi na kuwauliza maoni yao kuhusu kutolewa kwa ripoti hiyo.