Huwezi kusikiliza tena

Brazil iko tayari kwa dimba la dunia?

Shirikisho la Soka duniani FIFA limeonya kuwa mji wa Sao Paolo wa Brazil huenda ukanyimwa haki ya kuwa wenyeji wa mechi yoyote ile ya Kombe la Dunia mwakani kwa sababu ya ucheleweshaji katika ujenzi wa viwanja vya kandanda.

Huu ni utata mwingine mpya kughubika maandalizi ya Kombe la Dunia mwakani.

Anayeongoza ukosoaji huu ni Romario, aliyewahi kuwa mchezaji mahiri wa Brazil. Paul Nabiswa anatuarifu zaidi.