Huwezi kusikiliza tena

Uchafuzi wa mazingira Niger Delta

Uchafuzi wa mazingira unaotokana na mafuta ni tatizo linaloendelea eneo la Niger Delta nchini Nigeria, huku mashamba, maziwa na mito yakiharibiwa na mafuta yanayomwagika ovyo.

Uharibifu wa mali asili kwenye eneo hilo umewalazimisha watu wengi kuhama, kwenda kutafuta njia mbadala za kujikimu. Katika taarifa ifuatayo, Zawadi Machibya anaangazia maisha yalivyokuwa kabla ya makampuni makubwa ya mafuta kuingia Niger Delta.