Huwezi kusikiliza tena

Ajikimu kwa sanaa ya majeneza

Majeneza hutengezwa kwa miundo tofauti, inaweza kutengezwa kwa mbao ikiwa na mikono ya chuma na vyovyote vile. Lakini Nchini Ghana, mazishi huegemea sana katika kusherehekea maisha ya mtu na majeneza huundwa kwa urembo wa hali ya juu na nyingine huwa miundo ya kiajabu ajabu.

Muundaji mmoja mkuu wa majeneza alizuru Uingereza hivi karibuni na kuonyesha sanaa yake ya kutengeza majeneza na hata kutumai kuwa biashara yake inataweza kunawiri kwa kupata jicho la waingereza.