Maandamano zaidi kupinga wabunge Kenya

Mashirika yasiyo ya kiserikali yamefanya maandamano mwengine mjini Nirobi Kenya kupinga jaribio la wabunge kujiongeza misahahara hata baada ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kusema kuwa hakuna pesa za kutosha kuwaongeza misahara wabunge hao.

Mashirika hayo yanataka wabunge kukubali misahara waliyowekewa na tume ya kudhibiti mishahara ya wafanyakazi wa serikali. Kulingana na tume hiyo wabunge wanapaswa kupokea dola elfu sita kila mwezi lakini wanataka pesa hizo kuongezwa hadi zaidi ya dola elfu nane au shilingi laki nane za Kenya.