Huwezi kusikiliza tena

Polisi wakana kumshambulia Meya UG

Siku baada ya usiku wa tukio, Polisi nchini Uganda wamekanusha kuhusika na shambulio la bomu la machozi dhidi ya meya wa Kampala, Erias Lukwago. Meya anadai polisi walitumbukiza bomu ndani ya gari lake.

Akizungumza na BBC akiwa kitandani hospitalini, meya huyo Erias Lukwago, alisema alizirai baada ya gesi ya kutoa machozi ilipotupwa ndani ya gari lake tarehe 21 mwezi huu.

Anaeleza kwamba maafisa wa polisi walimpiga kifuani na kuzirarua nguo zake wakimshutumu kwa kuchochea ghasia.

Watu watatu walijeruhiwa na wengine kumi na wanne wamekamatwa. Siraj Kalyango anatuarifu kutoka Kampala.

Meya huyo ni mpinzani wa rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni.