Huwezi kusikiliza tena

Idadi ya wakimbizi yaongezeka Afrika

Kuna wakimbizi wa kisomali wapatao milioni nne duniani, na wengi wanakabiliwa na maisha magumu. Kuna wale wanaotumaini kurejea katika nchi yao ambako hali imeanza kutengamaa kufuatia miongo miwili ya mapigano ya kiukoo.

Lakini kwa wengine wengi, bado hawajui waende wapi baada ya kukaa ukimbizini kwa miaka mingi. Nchini Kenya inakadiriwa kuna wakimbizi wa Kisomali wapatao milioni moja. Mwandishi wa BBC Anne Soy ametembelea familia moja ya wakimbizi wa Kisomali.