Huwezi kusikiliza tena

Google matatani kwa kujipendelea

Kampuni ya Google haijatoa tamko lolote kujitetea dhidi ya tuhuma kuwa huwa ina mapendeleo zaidi wakati inapotoa matokeo ya tafutafuta kwenye mtandao wake, kulingana na afisaa mmoja kutoka Ulaya. Google imetoa mapendekezo kadhaa kufuatia wasiwasi kutoka kwa mkuu wa ushindani ulaya kwamba anataka Google kujizuia na hilo.

Google imejipata pabaya baada ya kupandisha hadhi ya programu yake ya ramani. Licha ya kuongeza programu kadhaa , inaonekana kufuta kisiwa cha Scotland cha Jura kutoka kwenye ramani yake na kuwacha barabara katikati ya bahari.