Huwezi kusikiliza tena

Watoto na mwezi wa Ramadhan

Mamilioni ya waislamu duniani wako katika mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhan. Ingawaje ni lazima kwa watu wazima, walio na afya nzuri kufunga, kuna msamaha kwa wagonjwa, waja wazito na wazee, angalau kwa muda.

Lakini kama waswahili wanavosema, samaki mkunje angali mbichi. Wazazi wengi wanawahamasisha watoto wao kufunga wakiwa bado wadogo. Je kuna wakati bora kuwaanzisha kufunga? Zuhura Yunus ametembelea jamii moja hapa london kuona inavyofanywa.