Huwezi kusikiliza tena

Kipindi cha lala salama Zimbabwe

Kampeni zinamalizika leo nchini Zimbabwe kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu siku ya Jumatano.

Chama cha Movement for Democratic Change cha waziri mkuu Morgan Tsvangirai kimefanya mkutano wake wa hadhara mjini Harare, huku Rais Robert Mugabe akizungumza na wafuasi wake jana.

Wawili hao wamekuwa katika serikali ya muungano tangu mwaka 2008. Hassan Mhelela ametuandalia taarifa hii kutoka Harare.