Huwezi kusikiliza tena

Mashindano ya riadha Moscow yabisha hodi

Maureen Chelagat ananuia kuiga mfano wa wakimbiaji wa zamani wa Afrika Mashariki mbio za mita mia nne za wanawake, Mkenya mwenzake Ruth Waithera na marehemu Judith Ayaa wa Uganda ambao walivuma sana nyakati zao kwenye mbio za mita mia nne, Waithera akivunja rekodi ya Ayaa ya Afrika Mashariki kwa kukimbia sekunde 51 nukta tano-sita katika michezo ya Olimpiki mwaka wa 1984 huko Los Angeles, Marekani.

Waithera hakuvunja tu rekodi hiyo bali alifuzu kwa fainali pia. Ayaa alikua anashikilia rekodi ya Afrika Mashariki ya sekunde 52 nukta sita-nane aliyokimbia kwenye michezo ya Olympiki mwaka wa 1972.

Hadi wa leo rekodi ya Waithera haijavunjwa. Maureen anataka kufanya vizuri zaidi ya Waithera na Ayaa atakapoiwakilisha Kenya katika mbio za dunia kuanzia Jumamosi ijayo mjini Moscow……JN amezungumza na Maureen katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi..