Huwezi kusikiliza tena

Wakenya wazindu mchezo wa Video

Image caption Mchezo wa video

Biashara ya michezo ya video ina thamani ya mabilioni ya dola kwa mwaka.

Sawa na filamu kubwa zinazozalisha pesa nyingi, kuzinduliwa kwa mchezo mpya wa video huwafanya mashabiki kuchanganyikiwa kwa furaha.

Soko la michezo hii limehodhiwa na makampuni kutoka Marekani na Asia ya mashariki.

Lakini Wesley Kirinya akiwa na mwenzake Eryam Tawia, waligundua kuwa kuna pengo la biashara hii barani Afrika na wakaanzisha michezo yao inajulikana kama Leti Games kuutumia mwanya huo.

Wesley Kirinya amezungumza nasi kuhusu michezo hiyo ya Video.