Huwezi kusikiliza tena

Msako dhidi ya wahamiaji haramu Tanzania

Zaidi ya watu sabini wanaodai kuwa ni raia wa Tanzania wamegoma kuendelea na safari kuingia nchini Rwanda baada ya vyombo vya dola nchini Tanzania kuwafikisha kwenye mpaka wa Rusumo kati ya mataifa mawili.

Awamu ya kuwaondosha kwa nguvu wamamiaji haramu kutoka Tanzania kwa agizo la rais Jakaya Kikwete imeanza mwishoni mwa juma,baada takriban wanyarwanda elfu saba kurejea hapo awali kwa hiari yao japo baadhi walidai kuyakimbia maskani yao kutokana navitisho kadha wa kadha dhidi yao.

Mwandishi wa BBC John alikwenda katika mpaka wa Rusumo kujionea hali