Huwezi kusikiliza tena

Wahamiaji haramu TZ waende wapi?

Mwezi Julai, Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete alitoa kauli kuwataka wahamiaji haramu wote kuondoka nchini humo kwa hiari ndani ya wiki mbili.

Yeyote atakayebakia baada ya muda huo angefukuzwa.

Hadi sasa wahamiaji haramu 25,000 kutoka Burundi, Rwanda, Uganda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Malawi wameshaondoka nchini humo.

Lakini hali imekuwa ni ngumu kwa wengi waliokuwa wakishi Tanzania kwa miongo kadhaa. Kutoka mkoa wa Kagera, Tanzania, mwandishi wetu Tulanana Bohela anatuelezea zaidi.