Huwezi kusikiliza tena

Rais Kenyatta: Sote tunaomboleza

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alihutubia taifa kufuatia shambulizi la kigaidi dhidi ya jengo la kifahari lenye maduka makubwa mjini Nairobi la Westgate. Kundi la Al Shabaab lilikiri kutekeleza mashambulizi hayo yaliyosababisha vifo vya watu 69 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 170 ikiwemo wanajeshi wanne.

Rasi Kenyatta aliahidi wakenya kuwa waliohusika na shambulizi hilo watakiona cha mtema kuni na kuwaeleza wakenya kuwa yuko pamoja nao katika kuomboleza kwani naye aliwapoteza jamaa zake kwenye shambulizi hilo.

Kenyatta lishirikiana na vioingozi wengine nchini Kenya kuwataka wakenya kuwa watulivu wakati maafisa wa usalama wakijaribu kufanya kila hali kuwaokoa mateka ambao bado wako ndani ya jengo hilo.

Hili ni shambulizi la kwanza la aina yake nchini Kenya na kwa mujibu wa kundi la kigaidi la Al Shabaab ni la kulipiza kisasi kwa Kenya kujihusisha na vita nchini Somalia.

Kufikia sasa polisi wa Kenya wanasema wamewakamata washukiwa wawili. Mmoja ambaye ni mkenya aliyebadilisha dini na kuwa muisilamu na hata kufanbyiwa mafunzo nchini Somalia na kundi la Al Shabaab. Taarifa zengine zinasema mshukliwa wa pili alikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimatafa wa Jomo Kenyatta akijaribu kukwepa kwenda Uturiki