Huwezi kusikiliza tena

Tukio la kushtua kwa wakenya

Baada ya siku tatu ya mashambulizi yaliyofanywa na magaidi katika jengo la Westgate mjini Nairobi, hali bado haijawa shwari. Maafisa wa usalama wanasema kuwa wamedhibiti hali, wakifanya msako katika jengo hilo kuwaondoa magaidi waliosalia humo ndani.

Wanasema kuwa wamewaua magaidi sita na kuwakamata wengine zaidi. Lakini duru zinasema kuwa kundi hilo linalodai kuwa wanachama wa kigaidi wa Al shabaab linasisitiza kuwa bado linawazuilia mateka zaidi.

Kufikia sasa idadi ya waliofariki ni sitini na wawili ingawa wengine 51 bado hawajulikani waliko.Wakati huohuo,waziri wa mambo ya nje wa Kenya anasema kuwa miongoni mwa magaidi hao ni wamarekani wawili au watatu na muingereza mmoja.

Uingereza na Marekani zinachunguza madai hayo. Ann Soi aliandaa taarifa hii