Huwezi kusikiliza tena

Red Cross:Uhalifu usituzwe michezoni

Kamati ya kimataifa ya Red Cross inataka kuwa na ushawishi mkubwa katika michezo ya kivita ya video.

Shirika hilo la misaada linasema kuwa masharti ya kivita yanapaswa kutumika katika michezo hiyo kwani inatengezwa kiasi cha kuonekana kuwa ni ya kweli wakati sio.

Linadai kuwa michezo kama Medal of Honour au Call of Duty inapaswa kuhakikisha kuwa vitendo ambavyo vinaonekana kama uhalifu wa kivita havituzwi katika michezo hiyo.