Huwezi kusikiliza tena

Je wewe huvalia nguo kuu kuu za ndani?

Je unaweza kununua na kuvalia nguo kuu kuu za ndani? Nguo nyingi zinazovaliwa katika mataifa yaliyostawi hujikuta kwenye masoko ya miji mbali mbali Afrika, ikiwa ni pamoja na chupi na sidiria.

Na walio wengi barani humo wanaziona nguo hizo ni za bei nafuu zaidi kuliko mpya zinazotengenezewa nchini mwao. baadhi ya nchi zimepiga marufuku uuzaji wa nguo kuu kuu za ndani.

Wazo la kupiga marufuku uuzaji wa nguo kuu kuu za ndani nchini Zimbabwe lililotolewa na aliyekuwa wakati mmoja waziri wa fedha Tendai Biti, aliyenukuliwa akisema:"Kama wewe ni mume na unamuona mkeo akinunua nguo za ndani sokoni, hapo utakuwa umeanguka mtihani."

Lakini Malawi bado zinauzwa kama anavyosimulia mwenzetu Ann Soy.