Huwezi kusikiliza tena

Utawala bora Afrika ni ndoto au?

Kwa mara nyingine hakupatikana mshindi wa tuzo ya Mo Ibrahim ya utawala bora.

Hii ni mara ya nne kamati inashindwa kupata mshindi anayepewa donge la dola milioni 5, kwa viongozi waliochaguliwa kidemokrasia na kun'gatuka madarakani kwa hiari barani Afrika.

Wakfu wa Mo Ibrahim ulianzishwa mwaka 2006 na mfanyabiashara wa Sudan, ambaye ni muasisi wa kampuni ya simu ya Celtel.

Lengo la wakfu huu ni kuenzi uongozi na utawala bora barani Afrika, ili kusaidia kuhamasisha mabadiliko yakinifu barani Afrika.