Huwezi kusikiliza tena

Wanawake mabaharia wa Mombasa Kenya

Licha ya kuwa na fursa nyingi za kiuchumi, fani ya ubaharia imezorota katika pwani ya Afrika Mashariki hali iliyowafanya mabaharia wakongwe kukata tamaa .

Imeripotiwa kuwa vijana wengi wanakataa kuwa mabaharia wakidai haina tija ya kutosha.

Lakini licha ya kutokuwa na meli binafsi sasa serikali ya kenya imezindua upya mitaala ya mafunzo ya ubaharia vyuoni.

Na kama alivyobaini mwenzetu Jamhuri Mwavyombo sasa akina dada wanaichangamkia fursa ya kupata elimu ya ubaharia.