Huwezi kusikiliza tena

Watoto wanusurika HIV Kenya

Umetajwa kuwa mradi uliofaulu zaidi wa kupambana na ukimwi barani Afrika, mpango wa kuzuia maambukizi kwa watoto.

Afrika sasa kuna kizazi cha watoto ambao wazazi wao wanaishi na virusi hivyo, lakini wenyewe hawakuvipata.

Mwaka uliopita takwimu za Umoja wa Mataifa zilionyesha maambukizi hayo yamepungua zaidi ya nusu ikilinganishwa na miaka kumi iliyopita.

Anne Soy alimtembelea mama mmoja jijini Nairobi aliyeweza kuzuia kumuambukiza mwanawe na virusi hivyo.