Huwezi kusikiliza tena

Tahadhari yatolewa Uganda

Wiki iliyopita Uganda imejikuta ikitoa tahadhari ya kutokea ugaidi nchini humo.

Serikali ya Uganda imetoa tahadhari kali na ubalozi wa Marekani mjini Kampala umewaonya raia wake uwezekano wa kutokea shambulio kama la maduka la Westgate jijini Nairobi, Kenya.

Uwanja wa raga uliolipuliwa na Al-Shabab mwaka 2010, uliandaa mashindano ya raga na ulifurika mamia ya watazamaji.

Zuhura Yunus anaripoti zaidi.