Huwezi kusikiliza tena

Botswana:Wanawake huru kurithi

Kwa wiki ya pili sasa BBC imekuwa ikonyesha makala maalum kuwaenzi wanawake, tukitazama mafanikio na changamoto wanazokabiliana nazo.

Mfululizo huu utafikia kilele Ijumaa ya wiki hii ambapo wanawake mia moja kutoka sehemu mbalimbali duniani watakuja hapa BBC kwa shughuli maalum.

Leo tunatazama suala la urithi. Mahakama moja nchini Botswana hivi karibuni imetoa haki ya kurithi kwa wanawake, na kutupilia mbali utamaduni wa wanaume kuwa ndio warithi wakuu wa mali. Zuhura Yunus anaarifu zaidi.