Huwezi kusikiliza tena

Maisha ya Lagos yanogeshwa ukumbini

Broadway mjini New York na London zinajulikana kwa michezo ya kuigiza yenye kutumia waigizaji na nyimbo tele na ambao unacheza kwa muda mrefu, lakini sifa hii imeingia Lagos. Je wanaweza kufika kiwango cha Uingereza na Marekani?

Mchezo wa kuigiza kwa nyimbo unaoonyeshwa katika kumbi za michezo ya kuigiza kwa jina Saro, umeanza kuonyeshwa mjini Lagos.

Ni mchezo wa kuigiza kuhusu wahamiaji waliohamia Lagos kutafuta maisha mazuri.

Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo alihudhuria uzinduzi rasmi wa mchezo huo Saro, ambao umesemekana kuweza kufungua upya ari ya watu kuanza kwenda katika kumbi za michezo ya kuigiza Nigeria.