Huwezi kusikiliza tena

Tanzania inasubiri nini?

Tanzania imesema bado inajipanga kabla ya kuungana na nchi nyingine za Afrika Mashariki katika kutoa visa za kusafiria za pamoja kwa watalii.

Wiki iliyopita, Kenya,Uganda, na Rwanda zilikubaliana kuwa na utaratubu huo utakaoanza kutumika mapema mwakani.

Watalii watahitaji kuchukua visa moja tu na kuweza kutembelea nchi hizo tatu, tofauti na zamani ambapo wageni walitakiwa kununua visa kwa kila nchi.

Je nini hasa ambacho Tanzania inasubiri? Swali hilo nimemuuliza naibu waziri wa Utalii wa Tanzania, Lazaro Nyalandu.