Huwezi kusikiliza tena

Je wako tayari kurejea Somalia?

Umoja wa mataifa hii leo unajitayarisha kuanza utafiti katika kambi mojawapo kubwa ya wakimbizi duniani Daadab kaskazini mwa Kenya kuchunguza ni kiasi gani cha wakimbizi takriban nusu milioni wa kisomali wapo tayari kurudi nchini mwao.

Wiki iliyopita serikali ya Kenya, Somalia pamoja na shirika la UNHCR, zilitia saini makubaliano ya kuwarudisha nyumbani wakimbizi hao.

Mwandishi wa BBC Bashkas Jugosdaaya alizuru kambi ya Daadab