Huwezi kusikiliza tena

Walaani Saudia kwa swala la wahamiaji

Mamia ya wa Ethiopia mjini London waliandamana nje ya ubalozi wa Mamlaka ya Saudia siku ya Jumatatu . Wengi wao walibeba mabango na kwa sauti kubwa kuiambia serikali ya Saudia, 'Aibu juu yenu'.

Saudia ilianza kuwakamata na kuwafunga au kuwarejesha maelfu ya wahamiaji wasio rasmi nchini humo wengi wao wakitoka mataifa ya Asia na Afrika.

Mpaka sasa serikali inasema watu laki tisa wamerejeshwa. Kassim Kayira alikuwa nje ya ubalozi wa Saudia mjini London.