Huwezi kusikiliza tena

Ndoto ya reli ya kasi Kenya!

Mizigo zaidi na kwa haraka zaidi- hiyo imekuwa ndoto kwa wafanyabiashara wengi barani Afrika.

Kumekuwa na malalamiko kuhusu kuchelewa kwa bidhaa na miundombinu mibovu kukwaza ukuaji wa uchumi.

Hii leo, Afrika Mashariki imeshuhudia kuanza kwa hatua ambayo huenda ikabadili yote hayo.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amezindua rasmi mradi wa reli katika jiji la Mombasa, utakaounganisha Kenya na Uganda, Sudan Kusini na Rwanda. Emmanuel Igunza amehudhuria uzinduzi huo.