Huwezi kusikiliza tena

Mandela Rambi Rambi zamiminika

Salamu za Rambi rambi zimeendelea kumiminika kutoka kwa kila aliyemfahamu Nelson Mandela, kama kiongozi, rafiki na jamaa.

Papa Francis, kiongozi wa kanisa katoliki, amesema atamuombea Mandela, hasa kwa kua alikuwa kiongozi aliyetetea sana maslahi ya wananchi na kutetea sana demokrasia na amani hasa nchini Afrika Kusini ambako alipigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa Rangi.

Naye Dalai Lama amesema kuwa ameshtushwa sana na kifo cha Mandela, na kuwataka watu kuendeleza sera zake.

Kiongozi mpigania demokrasia wa Burma, Aung San Suu Kyi, amesema kuwa Nelson Mandela alitetea sana haki za binadamu na usawa pamoja na utu kwa watu wote.

Rais wa Brazil, Dilma Rousseff, amesema mfano aliotoa Mandela, utatoa mwongozo kwa umma.

Naye waziri mkuu wa India, Manmohan Singh, alisema Mandela likuwa mtu mkubwa miongoni mwa watu wengi na mtu mkweli sana.