Blogu ya Mtayarishi

Image caption Meneja Mkuu Mtayarishi : Jackie Christie azungumzia maandalizi ya kipindi maalum.

Tukiwa tumeandaa vipindi zaidi ya 50, timu ya Sema Kenya imenyorosha uandalizi wa hiki kipindi cha telezisheni na redio. Hata hivyo, sio kwamba hii kazi ni rahisi. Kwa mfano, kazi ya kuwaalika jopo kwenye mjadala…

Katika kipindi chetu kilichopita, tuliandaa mjadala maalum kuambatana na miaka 50 ya uhuru Kenya. Watayarishi waliandika orodha ndefu ya washiriki wakiwa na matumaini kwamba watahudhuria. Wasomi, mawakili, wasanii, wapiganiaji uhuru, waandishi, wanaharakati na wengi wanaoshawishi maoni ya umma walitarajiwa kuhudhuria. Wengi waliochangia historia ya kisiasa na kijamii ya nchi na wengine walio na maoni mazito kuhusu jinsi nchi itakuwa katika siku za usoni. Nilifurahia orodha hiyo kabisa.

Lakini, kuwa na orodha ya washiriki ni kitu kimoja, kuhakikisha kwamba watahudhuria ni kitu kingine tofauti kabisa. Tukiwa na wiki chache tu, watayarishi na watafiti walianza kuwapigia simu viongozi waliowalenga.

Mwanzo

Image caption Washiriki katika kipindi maalum cha miaka 50 ya Kenya. Katikati: Evans Gor Semelang’o, Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo ya Biashara za Vijana.

Ufunguzi wa mazungumzo unaanza na maelezo mafupi ya Mheshimiwa

Kinachofuata ni maelezo zaidi kuhusu kipindi hiki na kusisitiza umuhimu wake katika huo mjadala. Baada ya hapo ni ziara - maeneo ambapo mjadala utafanyika kwani kipindi hiki kinazuru sehemu mbali mbaliu za Kenya.

Baada ya maandalizi kukamilika sasa ndipo swala kuu linaulizwa, ”Je, wajua kwamba kipindi kinaendeshwa kwa lugha ya Kiswahili?”

Wageni au viongozi huhitilafiana katika majibu yao au anaanza kwa kauli fulani na kadiri mjadala unavyoendelea ndivyo kauli nazo zinababilika.

Kuna viongozi wengine nao wanahitaji kubembelezwa, na Mtayarishi anakuwa na wakati mgumu akiwahakikishia viongozi kuwa la muhimu sio usanifu au ukwasi wa lugha . Mtayarishi akifanikiwa, katika majadala aliuandaa na kuona mambo yamekuwa muruwa, mtayarishi anacheza densi akisherehekea mafanikio!

Katika kipindi chetu cha kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wqa Kenya , tuliona kwamba asilimia kubwa ya walio na uwezo wa kuwa washiriki hawawezi kujieleza kwa ufasaha wakitumia lugha ya Kiswahili katika mjadala.

Lugha ya Taifa

Lugha ya kawaida ya kibiashara nchini Kenya ni Kiingereza, ingawa Kiswahili kinafunzwa shuleni kama lugha ya pili.

Hata hivyo, Wakenya wengi hutumia angalau lugha tatu: lugha ya mama, Kiingereza na Kiswahili. Vijana jijini Nairobi huchanganya Kiingereza na Kiswahili na kuzungumza lugha mchanganyiko wa sheng. Vijijini, Wakenya huzungumza lugha nyingi tofauti.

Miaka 50 ya Uhuru

Image caption Baadhi ya waliohudhuria mjadala

Kando na masuala ya lugha, timu ya waandalizi na jopo waliweza kuandaa mjadala maalum kuadhimisha miaka 50 ya uhuru nchini. Kipindi hiki kilikuwa chenye hisia nzito.

Muundo wa hiki kipindi kilikuwa tofauti. Badala ya washiriki kuuliza wajopo maswali, washiriki walipata nafasi ya kutafakari juu ya maendeleo Kenya na kuzingatia kama imefikia malengo ya uhuru baada ya miaka 50 ya kujitawala. Wakenya kutoka pembe zote za nchi wakiwemo wapiagniaji uhuru, waliopigania demokrasia ya vyama mbalimbali, wasanii na waandishi wa blogu walishiriki.

Juliani, mwanamuziki alievuma, alionekana akichana Kamusi kablwa ya kipindi ili ajieleze vyema zaidi.

Johnson Sakaja, mwenye kiti wa chama cha TNA kinachotawala nchi sasa hivi, alizungumza na mshiriki mwenzake ambae anakumbuka bendera ya wabeberu likishushwa na ya Kenya likiinuliwa pale Uhuru Park mwaka wa 1963.

Lugha ya Kawaida

Nimeishi Kenya kwa muda mrefu na huwa ninatafakari nikijiuliza ni kwa nini nashindwa kuzungumza Kiswahili. Wakenya wengine wakigundua kwamba mimi ni Mwingereza, huwa wanazungumza nami wakitumia Kiingereza chao fasaha. Ila tatizo kuu ni kwamba mimi sio mwanaisimu wa lugha, na hivi naishi katika jiji kuu Nairobi ambapo ni rahisi kujieleza nikitumia Kiingereza badala ya kutumia Kiswahili kibovu.

Labda baadhi ya hawa wana jopo wana tatizo sawa na mimi?

Kutozungumza Kiswahili haimaanishi kwamba Wakenya wametupilia mbali mila yao. Ninavyoona, Wakenya ni wabunifu tena wanapenda maendeleo. Kwa hivyo huwa wanatumia chochote ambacho kitawasaidia kujiendeleza. Kama ni Kiingereza, basi liwe liwalo wataiambata.

Kwa wakati huu sio ajabu kwamba wengi ninaokutana nao, kama vile wafanyi biashara na wachuuzi wameanza kujifunza Kichina- Ama kweli wakenya ni wabunifu!

Blogu hii iliandikwa kwanza katika blogu ya BBC Media Action.