Huwezi kusikiliza tena

Wenyeji wa Kalahari hatarini

Wenyeji wanaoishi katika mapori ya jangwa la Kalahari wapo hatarini kupoteza utamaduni wao.

Serikali nchini Botswana inawalazimisha kuanza maisha mapya katika kambi zilizopo mbali na maeneo yao ya asili, ambayo ni katika hifadhi ya wanyama ya Kalahari. Baada ya mvutano wa miaka 15 mahakamani na serikali, wenyeji wapatao 200 wameruhusiwa kurejea katika hifadhi.

Lakini wengi wanahitaji vibali na hawaruhusiwi kuwinda, na wanaokiuka, wanakamatwa. Omar Mutasa anatuarifu zaidi.