Huwezi kusikiliza tena

Nani alimuua Kanali Karegeya?

Balozi wa Rwanda nchini Afrika Kusini Vincent Karega ametetea matamshi ya waziri mkuu wa Rwanda kuhusu mauaji ya kanali Patrick Karegeya aliposema kuwa raia

anaesaliti taifa lake baada ya kuwa binadamu mwenye sifa kamili na kupewa maisha bora lazima siku zote atafikwa na kipigo.

Nae waziri wa mambo ya njee wa Rwanda Bi Louise Mushikiwabo akasema kanali Karegeya alijitangaza kuwa adui wa Rwanda

Alidhania atahurumiwa ? Yote hayo yalikua kwenye mtandao wa kijamii. Mwandishi Wetu Omar Mutasa amemuuliza balozi Karega hio inaonyesha kama Rwanda ilihusika na mauaji hayo ?