Huwezi kusikiliza tena

Haba na Haba TV Tanzania

Haba na Haba TV ni kipindi cha uhalisia, ukweli na kinachoangazia maisha halisi ya watu wa Tanzania katika mambo wanayokabilana nayo kila siku.

Dakika 30 za fursa muhimu kwa wananchi wa kawaida kabisa kujua mwenendo wa utawala bora katika nchi yao ya Tanzania kwa kuhoji viongozi wa nchi na wao kupaza sauti kwa kueleza simulizi za maisha yao ya kila siku na kisha viongozi wenye dhamana wakipata nafasi ya kujibu hoja zinazojitokeza.

Miongoni mwa mambo yanatojitokeza katika simulizi hizo ni pamoja na:- Maji na uhaba wa chakula, Ukosefu wa Ajira na umasikini, Barabara, Umeme, Rushwa, Elimu na Afya.

Makala hii pia hutazama mafanikio yaliyofikiwa na Serikali ya Tanzania kwenye huduma za kijamii nchini humo.

Tarehe za kurushwa hewani: January/ February 2014 kupitia Star TV. Pia unaweza kutizama vipindi hivyo kupitia kwenye mtandao wetu wa bbcswahili.com na pia kwenye simu yako ya mkononi