Huwezi kusikiliza tena

Ghasia za kidini zitakwisha CAR?

  • 10 Januari 2014

Rais wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Michel Djotodia,amejiuzulu mwishoni mwa mkutano wa kikanda nchini Chad ambao uliitishwa kutafuta suluhu kwa mgogoro wa kidini unaokumba nchi hiyo.

Bwana Djotodia amekosolewa kwa kukosa kutafuta suluhu ya kudumu kwa ghasia za kidini ambazo zimekumba taifa hilo tangu aingine mamlakani kwa njia ya mapinduzi.

Taarifa ya kujiuzulu kwa Djotodia imepokewa kwa shangwe sana na wakristo katika mji mkuu Bangui, ingawa upande wa waisilamu kumekuwa na kimya kikuu.

Michel Djotodia alikuwa rais wa kwanza mwislamu kuiongoza Jamhuri ya Afrika ya Kati. Tangu alipoingia madarakani, nchi hiyo imekumbwa na matatizo zaidi. Karibu watu milioni sita wamekimbia makazi yao, huku makundi mbalimbali yakiendelea kupigana. Alex Mureithi ana maelezo zaidi.