Huwezi kusikiliza tena

Buriani Komla Dumor

Mwandishi na mtangazaji mashuhuri wa BBC Komla Dumor ameaga dunia. Komla alifariki Jumamosi kutokana na mshtuko wa Moyo.

Wengi walimuenzi na watamkumbuka kwa kazi yake nzuri ikiwemo mahojiano aliyofanya na mwanawe hayati Nelson Mandela Bi Makaziwe, alivyotangaza shambulizi la kigaidi la Westgate mjini Nairobi na mengi aliyoyafanya katika kazi yake ya kila siku na BBC.