Huwezi kusikiliza tena

Mimi ni Al Shabaab

Mapema wiki hii Marekani ilifanya mashambulio ya makombora ndani ya Somalia yaliyomuua jasusi mkuu wa kundi la Alshaabab lenye uhusiano na mtandao wa al-Qaeda.

Shambulio hilo likiwa moja ya juhudi za vikosi vya Marekani na Afrika la kudhoofisha makundi ya jihad yaliyodai kuhusika na shambulio la mwezi Septemba dhidi ya jumba la westgate lililowauwa watu 67.

Al shabaab ilisema kuwa shambulio hilo lililenga kulipiza kisasi kwa majeshi ya Kenya yanayopigana Somalia dhidi yao.

Sasa Katika mahojiano ya kipekee na mwandishi wetu John Nene, Kijana mmoja wa Kenya amekiri kuwa ni gaidi na anadai amekuwa katika kundi la wanamgambo la Somalia la Al Shabaab tangu mwaka wa 2007 kutokana na matatizo ya kifedha.

Kijana huyo, ambaye alisilimu na kupewa jina la Mohammed, anaelezea sababu zinazowafanya vijana kujiunga na kundi hilo