Huwezi kusikiliza tena

Bilionea atunza watoto TZ

Kituo cha watoto mayatima mjini Arusha kina kila sababu ya kumshukuru billionea wa umri mdogo Zaidi nchini Tanzania, Patrick Ngowi, ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya umeme wa nishati Helvetic East Africa.

Mbali na kuwa mwanabiashara maarufu ambaye jina lake liko kwenye orodha ya watu tajiri zaidi ya Forbes, Ngowi, mwenye umri wa miaka 28, amejitokeza kuinua maisha ya vijana wa Tanzania kupitia miradi mbali mbali ya jamii.

Katika kazi zake kwa jamii Ngowi aliamua kumulika kituo cha watoto mayatima cha Arusha kwa kuwawekea umeme wa nishati ili wajiendeleze zaidi kimasomo na kimaisha kwa jumla…….

John Nene ametembelea kituo hicho na akatuandalia ripoti ifuatayo…