Huwezi kusikiliza tena

'Mvi hatari kwa usalama'

Je wafahamu kuwa na mvi katika baadhi ya sehemu katika pwani ya Kenya ni hatari kwa usalama na maisha yako?

Hilo limejitokeza huko Kilifi ambako wazee wamekuwa wakiuwawa na watu wasiojulikana kwa kisingizio kuwa ni wachawi.

Kutokana na hilo wazee wasiopungua thelathini wamekimbilia katika kaya iitwayo Godoma ili kuokoa maisha yao.

Kuna wazee wengine wanaodaiwa kuuawa kwa sababu za urithi na familia zao. Paul Nabiswa alikuwa Kilifi na kutuandalia taarifa zaidi