Huwezi kusikiliza tena

Sumu yaleta riziki Ghana

Mnamo mwaka 2012,dunia nzima ilizalisha tani milioni 49 za uchafu unaotokana na vifaa vya elektroniki vilivyotumiwa na itakapofika mwaka 2017, kiwango hicho kitafika tani milioni 65 kwa mwaka.

Lakini sheria mpya za Ulaya zilizoanza kutumika mwezi huu, zinalazimisha nchi za Ulaya kusaga angalau asilimia 45 vifaa vya elektroniki vilivyotumika nchini humo ili kuifanya kuwa vigumu kwao kuviuza katika nchi maskini.

Wakati huu, kiwango kikubwa cha uchafu huo, huishia katika nchi za Asia na Magharibi mwa Afrika ili kukaguliwa na wafanyakazi hasa watoto katika mazingira hatari sana kama inavyosimulia taarifa hii kutoka Ghana.