Huwezi kusikiliza tena

Ghana yamuaga Komla Dumor

Shughuli za mazishi ya rafiki yetu na mtangazaji mwenzetu Komla Dumor, aliyefariki dunia mwezi uliopita hapa London akiwa na umri wa miaka 41 zilifanyika mjini Ghana kuanzia Ijumaa na kumalizika Jumapili.

Taratibu za maziko ya Ghana zitachukua muda wa siku tatu.

Kulifanyika misa katika Kanisa Katoliki jijini Accra na baadae watu waliaga mwili. Ibada ya maziko ilifanyika mbele ya Ikulu ya Accra.

Rais wa Ghana, John Mahama, alimsifia Komla, ambapo alimwita mmoja wa mabalozi wazuri wa nchi hiyo. Zuhura Yunus anatuchukua hadi Accra kushuhudia yaliyotokea.